Kisuaheli / Ostafrika - SALA KWA YESU NA MARIA

_____________________________________________________

Kisuaheli / Ostafrika


Yesu! Maria! Ninawapenda

Muwe kitulizo chetu Mziokoe roho zote.

Amina.

Ee! Mioyo ya mapendo.

Ee! Mioyo iliyounganika kabisa katika mapendo.

Mnifanye niwapende ninyi kila wakati, na mnisaidie niwafanye wengine wawapende ninyi.

Muuchukue moyo wangu dhaifu wa kidhambi uwe ndani yenu,

na misinirudishie kamwe mpaka utakapokuwa mwali

wa moto wa mapendo yenu.


Najifahamu wazi kuwa sina hadhi ya kuja kwenu,

lakini mnichukue niwe ndani yenu,

na mnisafishe kwa moto wa mapendo yenu.

Mnichukue ndani yenu na mnitumie kama mnavyotaka ninyi,

kwani mimi ni mali yenu kabisa.

Amina.


Ewe! Mapendo safi!

Ewe!Mapendo matakatifu!

Mnichome kwa mishale ya mapendo yenu, na muiache damu yangu

imwagike ndani y madonda yeni yasiyokuwa na doa.

Ee! Mioyo isiyokuwa na doa!

Mniunganishe na mioyo yenu safi ili kunipa uhai wenu,

kunifariji, ili niwalukuze na kuwapenda. Amina.


Ee! Yesu! Ee!Maria!

Ninyi ni mioyo ya mapendo! Ninawapenda!

Mnitumie mimi kabisa

Mimi ni kafara yenu ya mapendo. Amina.


Ee! Mioyo ya mapendo!

Mnitumie mimi kabisa!

Mimi ni kafara yenu ya mapendo! Amina.


Imprimatur:

Tanzania / Njombe 1.8. 2004

Bishop Alfred Maluma of Njombe


Download

 
The last 100 visitors

beginn 05.11-2016